.

Jumamosi, 24 Desemba 2016

mastaa 8 walioushitua Ulimwengu baada ya kukiri ni waathirika wa Virusi vya Ukimwi.


Muigizaji Charlie Sheen  sio mtu maarufu wa kwanza kukiri haradhani kuwa anaishi na virusi  vya Ukimwi ila ni Staa aliefanya uamuzi huo kwenye karibuni baada ya kutamka kwa kinywa chake kuwa ni muathirika wa V.V.U alipofanya mahojiano na kipindi maarufu cha TV nchini Marekani kinachofahamika kama ‘TODAY SHOW’  mnamo November 17,mwaka 2016.
“I would like to admit that I am in fact HIV – positive,” he told Lauer. “I have to put a stop to this onslaught, this barrage of attacks and of sub-truths and very harmful and mercurial stories that are about me, that threaten the health of so many others and that couldn’t be further from the truth.”.Alisema na kuongeza alifanya makosa mengi hapo awali kwa kuwalipa watu kiasi kikubwa cha fedha ili kumtunzia siri hiyo.
2. Rock Hudson.
Muigizaji Rock Hudson ndiye mtu maarufu wa kwanza kukiri hadharani kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi baada ya kufikia uamuzi huo Julai 25 mwaka 1985.
Hata hivyo Hudson alifariki tarehe 2 ya  mwezi Oktoba,2016 akiwa na miaka 59,atakumbukwa kwa kuwasaidia watu maarufu wengi kufikia uamuzi huo wa kijasiri wa kukubali hali zao za kiafya.
Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa staa huyo wa Tamthilia maarufu ya ‘Pillow Talk’ aliambukizwa V.V.U akishiriki mapenzi ya jinsia moja.
3.Earvin ‘Magic’ Johnson.
Staa huyo wa zamani wa klabu ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya  Los Angeles (LA),alistaafu rasmi 1991 kushiriki ligi ya kikapu huku wakati huo akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kukiri kuwa alikua ameathirika na Vurusi Vya Ukimwi.
Johnson ambae kwa sasa ana miaka 56 amekua akiendesha kampeni ya elimu kwa jamii juu ya dhana potofu kuwa Ugojwa wa UKIMWI ni  ugojwa wa jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
4.Freddie Mercury.
Kwa mujibu wa swahiba wa Mercury anaefahamika kama Jim Hutton,Mwanamuziki huyo nguli wa miondoko ya R&B na Soul aligundua anaishi na V.V.U mapema kabla ya sherehe  za Pasaka mnamo mwaka 1987.ambapo baadhi ya vyombo vya habari vilianza kusambaza tetesi hizo.

Mnamo Novemba 23 mwaka 1993 alitoa andiko rasmi na kuthibitisha kuwa anaishi na virusi vya UKIWMI.
“I wish to confirm that I have been tested HIV positive and have AIDS. I felt it correct to keep this information private to date to protect the privacy of those around me.
“However, the time has come now for my friends and fans around the world to know the truth and I hope that everyone will join with me, my doctors and all those worldwide in the fight against this terrible disease.”.Ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo siku moja baada ya kutoka kwa taaarifa hiyo,Mercury alifariki dunia kwa maradhi ya Nimonia hii ikitokana kuwa muathirika wa Virusi Vya Ukimwi.
5.Eazy-E.Mnamo tarehe 24 ya  mwezi Februari mwaka 1995,rapper Erick Wright maarufu kama Ezzy- E alilazwa hospitali akiamini kuwa alikua akisumbuliwa na maradhi ya ‘Asthama’ ambapo baadae ilibanika kuwa alikua ameambukizwa Virusi Vya Ukimwi.
Eazy E ambae alikua memba wa kundi maarufu la HIP-HOP Ulimwenguni la N.W.A (Nig**r With Attitude) alidai kuwa alianza kufanya mapenzi akiwa na umri wa miaka 12 ambapo mpaka anafariki alikua na jumla ya watoto saba na wanawake saba tofauti.
Hata hivyo rapper huyo aliamua kufa na tai shingoni baada ya kugoma kukiri hali yake kiafya hadi taarifa ya maradhi yake kusomwa kwenye mazishi yake baada ya kifo chake mnamo tarehe 26 ya mwezi machi mwaka 1995.
“I just feel that I’ve got thousands and thousands of young fans that have to learn about what’s real when it comes to AIDS. Like the others before me, I would like to turn my own problem into something good that will reach out to all my homeboys and their kin. Because I want to save them before it’s too late,”.Ujumbe huo ulioandikwa na Eazy- E unaodaiwa kuandikwa na mkono wake ulisomwa siku ya mazishi yake na kuwaacha wapenzi wa mmuziki wa Hip Hop nchini Maekani na huzuni kutokana na kifo cha rapper huyo aliefarki akiwa na miaka 30.
6. Arthur Ashe.
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1980 mcheza tenisi maarufu Arthur Ashe aliaambukizwa Vizuri Vya Ukimwi baada ya kuongezewa damu ya mtu mwenye V.V.U.
Ashe anatajwa kama Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa kwanza kushinda taji la ubigwa w michuano ya tenisi la Wembledon na la US Open ambapo alifariki tarehe 6 ya mwezi February 1993.
7.Greg Louganis.
Louganis alibanika kuwa V.V.U mnamo mwaka 1988,ambapo mwaka 1996 mshindi huyo wa medali ya dhahabu ya michuano ya Olimpiki aliiushtua Ulimwengu baada ya kukiri kuwa alikua kishiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwa anaishi na V.V.U.
Hata hivyo amekua akishiriki kampeni za kuwasaidia waathirika wa UKIMWI ambapo mwezi Oktoba 2013 alifunga ndoa na mwenza wake Johnny Chaillot.
8.Liberace.
Mcheza Piano huyu maarufu alifariki mnamo mwaka 1987 huku akidaiwa kuwa alifanya siri juu ya hali yake kiafya.
Hata hivyo miezi kadhaa baada ya kifo chake daktari alithibitisha chanzo cha kifo cha Mwanamuziki na kudai kuwa alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi yatokanayo na UKIMWI.

SASA JIULIZE UNAFIKIRI KIBONGO-BONGO INAWEZA KUTOKEA SIKU MOJA STAA ANAEISHI NA V.V.U AKAKIRI HADHARANI…!? …THUBUTUUUUUUU……!!!

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wKpWorld https://m.youtube.com/channel/UClRfgiiKnP3u7JQ_Z4DPEHw

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni