.

Alhamisi, 10 Novemba 2016

Tuzo ya MTV EMA kurudi kwa King Kiba


MTV Europe music Awards 2016 ilifanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACTambayo ilitangazwa siku ya tukio mshindi ni Mnigeria Wizkid.
Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha Alikibandio anaongoza kwa kupigiwa kura na hapo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje? hata hivyo kulionekana mabadiliko baadae kwa rekodi hizo kutoonekana mtandaoni baada ya muda kupita.
Taarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.
Inaonekana Wizkid amefikiwa na taarifa na tayari post yake ya ushindi wa tuzo hiyo ameifuta kwenye mtandao wake, endelea kukaa karibu na kipax96.blogspot. com na HabNews Tv ili kila kinachonifikia nikufikishie, usisahau ku-SUBSCRIBE youtube channel ya HabNews Tv ili kupata matukio yote ya Tanzania kuanzia kwenye burudani, siasa, michezo na mengine.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni