.

Jumamosi, 5 Novemba 2016

Mr Nice Azungumzia Uvumi Ulioenea Kuwa Ana Ugonjwa wa Ukimwi

Gazeti la Taifa Leo la nchini lilifanya mahojiano na msanii mkongwe wa muziki wa Tanzania Mr Nice. Katika moja swali ambalo aliulizwa ni kuhusu tetesi ambazo zimesambaa nchini humo kuwa ana HIV. 

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, alikanusha uvumi huo huku akieleza nini kilimkuta mwaka jana mpaka akalazwa hospitali kwa miezi kadhaa. 

“Kaka wewe mwenyewe ukinicheki nilivyo fresh nina ngoma kweli?,” Mr Nice alimuuliza mwandishi huyo huku akicheka. “Siugui Ukimwi lakini ni kweli mwaka jana nililazwa hospitali kwa miezi mitatu kuanza October. Nililishwa sumu kali wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hatukuweza kubaini ni nani alifanya hivyo lakini tulijua ni mambo ya siasa na nikamwachia Mungu. 

Katika hatua nyingine Mr Nice alisema Tanzania kuwa na wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 kuliko jirani zake Kenya na Uganda kulitokana juhudi za msanii moja moja. 

“Kusema kweli wasanii wa Tanzania wamekuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri kuliko mwenzake. Kwahiyo binafsi naona hii hali imesaidia kuwajenga wasanii wa Tanzania pamoja na muziki kiujumla,”

Bonyeza HAPA kudownload application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni