.

Ijumaa, 4 Novemba 2016

Lil Wayne awaomba radhi mashabiki zake


Lil Wayne amewaomba msamaha mashabiki zake na watu wote baada ya kusema kwamba hazifahamu harakati za wamarekani weusi kupinga unyanyasaji unaofanywa na polisi “Black Lives Matter”.
Kupitia mtandao wa Tmz umeripoti kwamba Lil Wayne aliongea na mtandao huo kuwaomba msamaha watu wote ambao waliguswa na kauli yake aliyoiongea kuhusu Black Lives Matter, kikubwa ambacho kilimfanya kujibu vile ni pale mwandishi alipomuuliza kuhusu ishu ya mwanae wa kike kuitwa malaya, hapo ndipo alipoteza mood yote na kuamua kujibu anavyotaka yeye.
Wayne alisema yeye ni mtu mweusi na Tajiri Marekani, hio inatosha kujua maisha yake ni muhimu, mtu mweupe ndio anarekodi hio interview , anamrekodi mtu mweusi kwahiio maisha yake ni muhimu.
Alimalizia kwa kusema sijihusishi na jambo ambalo halinihusu wala kuniongelea mimi….. Ila baadae kwenye tamasha kubwa la muziki Rapa huyu alifuta kauli yake na kutoa maneno kuhusu harakati za Black Lives Matter kwenye Stage na kupata shangwe kubwa.
“When the reporter began asking me questions about my daughter being labeled a bitch and a hoe, I got agitated From there, there was no thought put into her questions and my responses.”


Download application yetu HAPA kwa habari kemkem

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni