.

Jumatatu, 14 Novemba 2016

King Kiba azungumzia ishu yake na Hakeem 5

Stori hii ilianza baada ya Abby Skills kusema Hakeem 5 lazima amuombe msamaha Ali Kiba ili wafanye kazi tena na mambo yake yaende sawa. 

Ali Kiba alisema “Kuhusu Hakeem 5, naweza kusema kwanza ni ndugu yangu kama Abby Skills na wengine. Tunaheshimiana nae sana. Sina ugomvi nae, tumefanya kazi nae kwa mapenzi yote tulipokuwa lebo moja G-records 

Kuhusu colabo na kutofanya video ya wimbo wa Hakeem 5 Kiba anasema “Ishu ipo hivi, nakumbukuka kabla sijapumzika kimuziki kipindi kile tulifanya kazi na Hakeem 5, nakumbuka ilikuwa inaitwa MADEBE. Baada ya kuitoa ilifanya vizuri, then nikaamua kupumzika miaka mitatu. 

Niliporudi rasmi akanifata tufanye video! Nikamwambia kweli?? Upo serious! Yani nyimbo ina miaka, then tuifanye video kweli. Ni Unprofessional kwa kweli.” 
Kuhusu kufanya nae colabo tena, Kiba aliniambia “Sitaki kufanya nae tena nyimbo, sijamkosea Hakeem lakini sitakuja kufanya nae kazi.”.

Bonyeza HAPA kudownload application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni