Hakuna asiyejua kuwa Salome ni wimbo mkubwa sana Afrika nzima kwasasa, na umesikika ukivunja rekodi kadhaa za video za muziki Afrika hasa katika mtandao wa Youtube. Ni wimbo ambao umepata mafanikio makubwa sana kwa muda mfupi tu baada ya kuachiwa.
Ukiachana na mafanikio ya wimbo, Salome imekuwa ni kama njia ya mafanikio kwa Raymond msanii ambaye ameshiriki katika wimbo huo kutusua kimataifa na kupata dili kadhaa katika nchi tofauti tofauti.
Akiongea na E-news ya EATV Raymondamethibitisha kuwa Salome imemfanya kupata shows kadhaa katika mataifa tofauti tofauti makubwa duniani.
“Nimeshapata booking nyingi sana za shows za nje hadi sasa, nimepigiwa simu India, nimepigiwa simu Italy na hata Marekani pia, na wote wanataka shows.”
Raymond aliisanua E-News kuwa Salome haikuishia kwenye Shows tu, bali hadi sasa amekwishafanya collabo kadhaa na wasanii wa kimataifa na kuwaahidi mashabiki zake wakae mkao wa kula muda wowote vyuma vinaachiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni