.

Jumatano, 12 Oktoba 2016

Sallam Sk afunguka kuhusu shutuma za Alikiba juu yake

Story iliyomake headlines kinoma noma weekend hii ni ile ya Salaam SK meneja wa msanii Diamond Platnumz kuhusishwa kuwa fundi mitambo katika show ya Mombasa Rocks Music Festival ambayo ilifanyika pande za Mombasa nchini Kenya na kumdondosha staa wa Marekani Chris Brown.
Kitu ambacho kilizua gumzo kinoma noma katika show hiyo ni pale Alikiba alipozimiwa mic na kutakiwa ashuke kwenye steji ili apande Chris Brown. Na baadae Alikiba alipoulizwa ni kitu gani kilisababisha yeye kushushwa kwenye steji alionyesha kutilia mashaka uwepo wa Sallam SKbackstage wakati yeye akiperform, na kudai kuwa huenda ni figisu figisu za meneja huyo wa Diamondndio zilisababisha yeye kufanyiwa kitendo kile.
Story hiyo imekuwa kubwa sana Afrika Mashariki kwa ujumla na kuzua maswali mengi ya sintofahamu kutokana na muhusika mkuu Sallam SK kutosikika akiongelea chochote kuhusiana na suala hili. HabNews inakuletea exclusive interview ambayo meneja Sallam SK amefanya na mtangazaji mkali nchini kenya Willy M. Tuva katika kipindi cha Mseto cha Radio Citizen.
Sallam amefunguka mengi sana juu ya tuhuma hizo na kudai kuwa Alikiba amekuwa akifanya kila njama kuhakikisha analiharibu soko muziki wa msaniiDiamond Platnumz katika sehemu tofauti tofauti, na hivyo kudai kuwa hizo ni njama za Alikiba kutakaDiamond achukiwe na watu wa Kenya kitu ambacho sio kizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni