.

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Povu la Eddy Kenzo kwa MTV

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Eddy Kenzo ameziponda tuzo za MTV Mama Awards, 2016 kwa kudai kuwa zilitolewa kwa upendeleo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Kenzo ambae ni mshindi wa tuzo ya BET-Viwers Choice Awards amedai kuwa waandaji kuna namna wanaifanya kuamua washindi wa MTV Mama na si upigaji wa kura maana kwenye kipengele chake yeye ndio alikuwa na kura nyingi akifuatiwa na Mr Flavour huku alieshinda ni Casper nyovest alikuwa na tatu kwa wingi wa kura.
Through his instagram Eddy Kenzo akawafungukia MTV Base, ujumbe huo ulisomeka hivi..
Tafsiri ya kile alichokiandika
“Mimi Balozi wa mtandao wa Simu wa Airtel, Bahati mbaya mtandao wa Simu wa MTN ndo wadhamini wa TuZo za Mtv Mama 2016 na Mshindi ktk kipengele nilichotajwa Ni Balozi wa MTN.
Eddy Kenzo akaendelea kutoboa
“kumbuka nimetumbuiza ktk nchi 35 na nchi 10 Kati ya hizo nimetumbuiza nikiwa na nyomi la Kwenye Viwanja vya Mpira, kuna nini, mafanikio gani Zaidi ya hayo? Eddy alihoji.
“Walituambia tupige Kura na Mashabiki zangu walifanya hivyo Kwa kwenda kwenye mitandao ya MTV, Eddy Kenzo akasisitiza
“Nenda Kwenye mtandao wao na bonyeza kipengele Cha #BestLiveAct na ukajionee Mshindi nani, sina wivu mimi Kama Jux ðŸ™ˆ) Ila nalalamika kwa sababu walituambia tupige Kura na mashabiki wakafanya maamuzi, nenda Kwenye page ya MTV ukaangalie walichosema, Hata Kwenye Emails, mimi Eddy Kenzo ndo niliyepigiwa Kura zaidi ya wote katika kipengele Cha Best Live Act na Msanii Ston Boy alikua wa Pili, Mr Flavour alikua wa Tatu, Na Casper Nyovest alikua wa Nne katika Platforms zote MTV Base Africa, lakini mwisho wa siku mtu wa 4 ndio amepewa Tuzo, jamani jamani hata ingekua wewe Povu lingekutoka tu, au mimi sikuwaelewa waliposema tupige Kura Kwa Msanii unayempenda? Eddy Kenzo akamalizia Kwa kuwashukuru mashabiki zake Na Mwenyezi Mungu.

Eddy Kenzo
Tuje kwenye uelewa zaidi, Nini alichomaanisha Eddy Kenzo
Kwa anachokimaanisha Eddy Kenzo ni kuwa wasanii Kama Navy Kenzo hata wangefanya nini wasingepata Tuzo kwa sababu eti kisa ni mabalozi wa AIRTEL Tanzania, pia Bwana Diamond Platnumz asingeweza kupata Tuzo kwa sababu yeye ni Balozi wa Vodacom, Yamoto Band na AliKiba nao wasingeweza kupata Tuzo kwa sababu ni mabalozi wa mtandao wa Simu.
Je kushindwa kwa wasanii wetu hapa nyumbani kuliangaliwa vitu hivi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni