.

Jumatano, 26 Oktoba 2016

Matonya akanusha kuhusu kukacha mkwanja wa kukodi ndinga


Naamini umeshafanikiwa kukitupia jicho kichupa kipya cha msanii Matonya kinachoitwa “Sugua Benchi”.
Ni kichupa flani hv kikali ambacho kimepata mapokezi mazuri ukiangalia na ukimya ambao alikuwa nao msanii Matonya kabla ya kuachia kichupa hicho.
Ndani ya kichupa hicho kuna ndinga flani hv kali aina ya BMW Kibanda wazi ambayo inaonekana humo ndani mtu mzima Matonya akila nayo bata na vitu kama hivyo.
Sasa taarifa kutoka Shilawadu zinadai kwamba inasemekana msanii Matonya hajalipia pesa ambayo walikubaliana na wamiliki wa gari hilo kulipa kama gharama za ukodishaji wa gari hilo.Soudy Brown amepokea simu kutoka kwa Tidoambaye ni muhusika wa gari hilo na kulithibitisha suala hilo.
Soudy Brown aliamua kumvutia waya Matonya na kutaka kumuuliza juu ya hili, cha ajabu ni kwambaMatonya amekanusha vikali tuhuma hizo na akidai kuwa kila kilichotumika katika video ile ni mali ya familia yake na wala hakuwa na sababu ya kulipia pesa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni