.

Ijumaa, 21 Oktoba 2016

Kanye West afunguka kuhusu bif la Apple na Tidal


Rapper Kanye West ameonekana kuchukizwa na figisufigisu zinazoendelea kati ya kampuni ya Tidal na Apple Music.
Kanye West ameamua kufunguka kwa mashabiki zake katika Tour yake ya Saint Pablo kwa kuwaambia kwamba hakutakuwa na mwendelezo tena wa “Watch The Throne 2” kutokana na bifu ambalo linaendelea la Apple Music na Tidal, Kanye pia alifunguka kuhusiana na ngoma ya Drake ya “Pop Style” na kuizungumzia kwamba mara kibao anapokuwa anataka kuperforme ngoma hiyo huwa Tidal inamzuia kutokana na ngoma hiyo inapatikana katika mtandao wa kustream ngoma wa Apple Music.
Hata hivyo Kanye alisema kwamba hakutegemea kuiona ngoma ya Pop Style kutoka bila ya verse zake kwani alihusika kwa asilimia kubwa, ila kilichokuja kutokea ni kuhusu kutokuelewana kwa Tidal na Apple.
“It will never be a Watch The Throne 2 You know why? Because that’s the reason why I wasn’t on the song. I wasn’t on the song cause of Hov. Cause it’s this TIDAL/Apple bullshit. And this shit be getting me tight every time I perform this muthafucka.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni