.

Jumatatu, 17 Oktoba 2016

Inasemekana nyumba aliyodai Da Prince na Naj ni yao inamilikiwa na wakwe


Kwa wengi haikuwa rahisi kuamini maneno ya Barakah The Prince kuwa anamalizia kujenga mjengo wake aliouonesha kwenye Instagram.

Ni kwa sababu ujenzi si suala la lelemama na linaloweza kutokea kwa usiku mmoja. Pia wengi walitia shaka uwezo wa msanii huyo katika kipindi hiki kuweza kujenga nyumba kama hiyo. Na sasa huenda mashaka hayo yakawa yamepata uthibitisho wa uhakika.

Ni kutoka kwa Alawi Junior – msanii wa Bongo Flava aliyemuoa na kuzaa na dada yake Naj, Lady Naa. Alawi amepost Instagram video ya nyumba ambayo Barakah alidai ni ya kwake na kuandika: Done🏠👍Hongera sana Mama mkwe #zaharaDattan nyumba yako kali sana.”
Alawi Junior (katikati) akiwa na shemeji yake, Naj (kushoto) mwenye uhusiano na Barakah

Cha kufurahisha ni kuwa Barakah na mpenzi wake Naj Dattan walihojiwa na EATV na wote kuthibitisha kuwa ni nyumba ya Barakah!
“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha E-Newz cha EATV.

Swali ni kama maneno ya Alawi ni ya kweli, kwanini Barakah anadanganya?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni