.

Jumapili, 4 Septemba 2016

MDUKUZI WA WATU MAARUFU MARCEL LAZAR AKAMATWA MAREKANI

Marcel Lazar aka Guccifer Hacker Facing Criminal Charges
Mahakama moja nchini Marekani imemfunga jela raia moja mwenye asili ya nchini Romania kwa kosa la udukuzi mtandaoni kwa watu wenye hadhi za juu nchini humo ikiwemo familia ya Bush.
Marcel Lazar, alikuwa akitumia mfumo wa “Guccifer”, kutekeleza udukuzi huo, amefungwa jela kwa muda wa miezi hamsini na mbili. Mwendesha mashtaka alisema Marcel aliidukua akaunti ya barua pepe ya Familia ya Bush naku baini picha binafsi zenye kushikamana na marais wa zamani, George H.W.Bush na George W. Bush.
Wakati wa mahojiano na mtuhumiwa huyo, alisema alivunja mfumo wa komputa binafsi uliokuwa ukitumiwa na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic Hillary Clinton, wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, hata hivyo kitengo cha usalama wa kimtandao nchini humo umepinga madai hayo.
Marcel alifikishwa nchini Marekani mwezi Aprili na kukutwa na hatia ya kuingilia mifumo binafsi ya watu ya komputa zilizokuwa na ulinzi binafsi.
Tabia hii imekithiri na Bongo pia kwa maana,
Johmakini amekuwa miongoni mwa marapa wachache sana bongo kufikisha followers milioni moja kwenye #Instagram ambapo amewashukuru mashabiki wake kwa sapoti wanayompa.
Hata hivyo account hiyo imeshachukuliwa na maharamia wa mtandaoni mara mbili. Joh amesema kwasasa amehakikisha anashirikiana na wataalamu wa teknolojia ya mitandao ili kuhakikisha anailinda.
Nay wa mitego pia ana zaidi ya followers milioni 1.wasanii wengi wenye zaidi ya followers milioni moja bongo ni waimbaji na waigizaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni