Stori Mbaya kunako industry ya burudani jana ni ishu ya mkali wa movie za Hollywood mwanamama Angelina Jolie kuomba talaka kwa baba watoto wake ambae pia ni muigizaji mwenzake Brad Pitt kwa kile anachodai ni kuboresha zaidi malezi ya watoto wao sita.
Moja kwa moja kuna baadhi ya mashabiki wa couple ya waigizaji hao wameonyesha kuvunjika moyo na kutokua na imani nao tena moja kati ya watu walionyeshwa kusikitishwa zaidi maamuzi hayo ni Christine Teigen (Mke wa John Legend) ambae kupitia ukurasa wake wa twitter Christine ameandika.
“Brad na Angelina, Nawezaje Kufanya Kazi Leo?”
Angelina Jolie amemshtumu mume wake Brad Pitt kwa kuwalea watoto wao malezi wasiyostahili, hivyo lengo lake kubwa ni kutaka kuwaweka watoto hao mbali na baba yao mpaka hapo atakapowaona kwa ruhusa maalum.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni