.

Jumanne, 23 Agosti 2016

RAYMOND AZAWADIWA GARI NA MANAGEMENT YAKE KAMA ZAWADI YA BIRTHDAY

Jana August 22 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya msaniiRaymond (Rayvanny) kutoka WCB Wasafi.
Usiku wa jana ilibidi ifanyike Party ya kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa msanii huyo pande za Madale nyumbani kwa msanii Diamond Platnumz. Ndipo uongozi mzima wa WCB ulipochukua uamuzi wa kumzawadia msanii huyo gari kama zawadi katika siku yake hiyo muhimu.
Siku zote huwa naamini juhudi za mtu ndio njia pekee ya kumfikisha mtu sehemu ambayo anaitaka endapo tu ataamini kwa kile ambacho anakifanya. Wote tumezishuhudia juhudi za msanii Raymondmpaka leo kufika hapa alipo tangu alipotokea katika mikono ya Clouds Media Group na kuelekea Tiptop Connectio na hadi sasa yuko WCB Wasafi lakini bado hakukata tamaa hadi leo wakati wake wa mafanikio umewadia.
Kila la khri kwa Raymond na mazuri mengine mengi yaendelee kumiminika ili apate nguvu zaidi ya kuendelea kutuletea muziki mzuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni