.

Jumanne, 23 Agosti 2016

Mtanzania aliyemaliza wa mwisho Olimpiki ya 1968

 Aliyekuwa mwanariadha wa Tanzania John Stephen Akhwari anakumbukwa kwa kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 1968 nchini Mexico.
Anajulikana kwa kuwa wa mwisho kuwahi kutokea katika michezo hiyo ya Olimpiki.Alimaliza wa mwisho saa moja baada ya wanariadha wenzake kumaliza.
Aliingia katika uwanja wa michezo akipepesuka huku akitokwa damu mbali na bendeji zilizokuwa katika mguu wake.
Alimuambia mwandishi wa BBC Sammy Awami kwa nini hakusalimu amri katika mbio hizo.
''Taifa langu halikunituma Mexico kuanza mbio bali kumaliza.Ni kutaka kwangu na uzalendo nilionao katika maisha yangu kama mwanariadha ndio ulionifanya kumaliza mbio hizo.
Licha ya kuwa nilikuwa na mauamivu mengi''.
Anaelezea kuwa mataifa mengine yaliwalinda wanariadha wao lakini hakuna mtu aliyemjali kwa kuwakilisha taifa lake.

John sasa ni mkulima na anaangazia ushiriki wake katika michezo hiyo.
''Ni fahari kubwa kwangu kushiriki katika mbio za marathon mjini Athns,Ugiriki mwaka 1962.
Nilikuwa wa pili katika mbio hizo,na shindano la pili lilikuwa lile la mwaka 1968 nchini Mexico''.
Kuhusu matokeo ya Tanzania ya michezo ya Olimpiki ya Rio De Janeiro,anasema:Nahisi vibaya lakini nifanyeje.Viongozi wa michezo hawawezi kubadili matokeo hayo.
''Iwapo timu yako haikushinda katika mashindano ya mwaka huu,ni lazima utafute njia za kuimarika ili uweze kushinda mwaka ujao na kuleta heshima kwa taifa lako''.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni