.

Jumatatu, 1 Agosti 2016

HII HAPA MISTARI AMBAYO NAY WA MITEGO ALITAKIWA KUIBADILISHA KWENYE “PALE KATI”





Moja kati ya adhabu ambazo tulizisikia alipewa mshkaji wetu Nay wa Mitego baada ya kufungiwa na BASATA ni ile ya kubadilisha baadhi ya mistari katika wimbo wake wa “Pale Kati”.
Sasa leo repper Nay wa Mitego amesema na sisi ni mistari gani ambayo BASATA walimtaka kuibadilisha katika wimbo wake.
“Kuna sehemu zilikuwa tatizo kwa upande wao lakini tulivyo kaa wakaweza kuzitaja, wakadai kwamba zinafumbua fumbo lililopo wakati katika sanaa siku zote msanii tu ndiye anaetakiwa kujua maana ya kitu alicho kiandika. Kuna sehemu ilikuwa inasema `Mwenye njaa na mademu’ hiyo imetolewa, pia kuna ile Kuna sample za mademu wenye vipara' nayo pia imetolewa, Nikilala napita na shem’, Hata demu wako pia ni wetu sote’, na hizo sehemu pia zimetoka. Nadhani ni sehemu kama tatu au nne hivi ndio zimebadilishwa.Ila sehemu kama Kitumbua na Mua ni sehemu ambazo nimezungumzia kama vyakula kwasababu vyote ni vitamu.” Alizungumza Nay wa Mitego

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni