Muziki umekuwa ni biashara kubwa sana siku hizi, Muziki umekuwa chanzo kikubwa cha kujipatia pesa na umaarufu kwa vijana wengi siku za karibuni.
Na hii ndio list ya wasanii 20 matajiri zaidi nchini Nigeria.
- 20. Patoranking

Ikiwa ngoma ya Garlie O ambayo kafanya na mwanadada Tiwa Savage ndio ngoma ambayo inasemekana imempa mafanikio makubwa sana king huyo wa dancahall na kumuingiza vizuri kwenye ramani ya muziki kimataifa, Anakadiriwa kumiliki zaidi ya pesa za ki-Nigeria (Naira) million mia tatu na hamsini. (N350,000,000)
- 19. Olamide

Boss wa YBNL Nation lebo ambayo inamiliki wasanii kadhaa wanaofanya poa sana nchini Nigeria, Olamide anashika nafasi ya 19 kwa kukadiriwa kumiliki zaidi ya pesa za ki Nigeria million mia tano na sitini. (N560,000,000).
- 18. Chidinma Ekile

Tumemsikia kwenye Perfect Combo ya Joh Makini mwanadada huyu, kikwao kwao anatajwa kuwa mmoja kati ya wanadada wenye mkwanja mrefu zaidi kati ya wale wanaoingiza mtonyo kupitia muziki. Anakadiriwa kumiliki zaidi ya pesa za ki-Nigeria millioni mia tano sabini na mbili (N572,000,000).
- 17. Duncan Mighty

Amesikika kwenye ngoma kama “Jide Ofo” ambayo kampa shavu rapper Phyno ambaye pia ni mnigeria. Duncan Mighty anakadiriwa kumiliki zaidi N700,000,000
- 16. Yemi Alade

Mwanadada ambaye huwezi kuacha kumtaja endapo utawatafuta wanadada ambao wanafanya poa sana katika music industry barani Africa. Tume enjoy hits zake kama “Johny, Kissing, Pose na nyingine kibaao. Anatajwa kumiliki zaidi ya pesa za kinigeria million mia nane na ishirini (N820,000,000).
- 15. Ice Prince

Amewahi kusikika kwenye collabo ya “Leo Leo” ya mwanadada Jokate wa hapa Tanzania. Ice Prince anatajwa kumiliki zaidi ya pesa za kinigeria million mia nane na sabini. (N870,000,000).
- 14. Phyno

Rapper mkali kinoma noma yan nchini humo na ngoma yake ya Fada Fada ambayo kafanya na Olamide inaendelea kufanya poa mpaka sasa katika media mbali mbali barani Africa. Anatajwa kumiliki zaidi ya N900,000,000.
- 13. Tiwa Savage

Akiwa chini ya lebo ya ROC Nation ya mtu mzima Jay Z ambayo amejiunga wiki kadhaa zilizopita, mwanadada Tiwa Savage kikwao kwao anatajwa kumiliki zaidi ya pesa za kinigeria million mia tisa na sabini (N970,000,000).
- 12. Kcee

Hit maker wa ngoma ya “LOve Boat” ambayo kaisuka na mnyama mkali kutoka Tz Diamond Platnumz, Kcee yeye anatajwa kushika nafasi ya 12 kwa kumiliki zaidi ya 983,000,000 ya pesa za kinigeria (N983,000,000).
- 11. M.I

Tumemsikia kwenye Demo ya ngoma ya “Aje” ya Alikiba, anatajwa kushika nafasi ya 11 kwa kumiliki zaidi ya million 988 ya pesa za kinigeria. (N988,000,000)
- 10. Timaya

Video yake ya “Money” ambayo kamshirikisha Mr Flavour ina viewers zaidi ya 2m hadi sasa ikiwa ina muda wa miezi 3 toka apandishwe katika mtandao wa Youtube. Timaya anashika nafasi ya kumi kwa kutajwa kumiliki zaidi ya Billion 1.1 ya pesa za kinigeria. (N1,100,000,000).
- 09. Banky W

Ametajwa kumiliki zaidi ya Billion 1.8 na kushika nafasi ya 9 katika list hiyo ya wanamuziki wanaomiliki mkwanja mrefu zaidi nchini Nigeria (N1,800,000,000).
- 08. Wizkid

Mmoja kati ya wanaharakati wanao pigania kuupeleka muziki wa Africa kwenye uso wa Dunia Wizkid, mwenye hit song kibao katika historia ya muziki wa Africa. Ametajwa kumiliki zaidi ya Billion 2.3 ya pesa za kiningeria. (N2,300,000,000).
- 07. Iyanya

Mr Oreo ni moja kati ya videos kali za msanii Iyanya ikiwa imefikisha viewers zaidi ya 3m katika mtandao wa Youtube, pia tulimshuhudia kwenye Bum Bum na Nakupenda zote akiwa amefanya na Diamond Platnumz. Ametajwa kumiliki zaidi ya Billion 2.5 za kinigeria. (N2,500,000,000).
- 06. Davido

Davido Adede Adedeke ndio jina kamili la hit maker wa “Skelew”, akiwa anasimamiwa na Sony Music Worldwide Davido ametajwa kushika nafasi ya sita kwa kumiliki zaidi ya Billion 2.9 za kinigeria. (N2,900,000,000).
- 05. 2 Face

Ni mmoja kati ya wanaqmuziki ambao wana mchango mkubwa sana katika muziki wa Nigeria kutokana na yeye kuwa kati wanamuziki wa zamani waliofanya vizuri kwa ngoma kama African Queen. Anatajwa kumilki zaidi ya Billion 4.5 za kinigeria, (N4,500,000,000).
- 04. D’Banj

Alisikika kuwa chini ya lebo ya Good Music ya mtu mzima Kanye West, D’ Banj ametajwa kumilikizaidi ya Billion 5 za kkinigeria (5,000,000,000)
- 03. Flavour

Tulimsikia kwenye Nana ya Diamond Platnumz, amekamata namba 3 ya washkaji wenye mtonyo mrefu kupitia muziki nchini Nigeria na anatajwa kumiliki zaidi ya Billion 5.7 (N5,700,000,000).
- 02. Don Jazzy

Mavin Records ni lebo ambayo inawamiliki wasanii kama Korede Bello, Di’ja na wengineo. kiongozi wa lebo hiyo ni Don Jazzy, mshkaji ambaye ndiye ametajwa kwenye nafasi ya pili kwa kumiliki zaidi ya Billion 7 za kinigeria (N7,000,000,000).
- 01. P Square

Ndio vinara kwa kumiliki mtonyo mrefu nchini Nigeria ambao wanasadikika kumiliki zaidi ya Billioni 25 za kinigeria (N25,000,000,000)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni