.

Alhamisi, 4 Agosti 2016

HAWA NI WATU WAWILI AMBAO DIAMOND PLATNUMZ ANATAMANI KUONANA NAO HAPA BONGO

Mwanamuziki Diamond Platnumz anaye fanya vizuri kwa sasa na ngoma aliyowashirikisha mapacha wawili kutoka Nigeria ambao ni P Square. Agosti 2 katika mahojiano na kituo cha redio CloudsFm aliweza kuulizwa vitu vingi na kuvitolea ufafanuzi zaidi juu ya hayo maswali aliyoweza kuuliza.
Mchongo huu hapa.. Hili ni moja ya swali aliloweza kuulizwa Diamond Platnumz.
Tayari umefanikiwa kukutana na watu wengi duniani, watu wa tasnia mbalimbali, ukipata nafasi ya kukutana na watu wawili Tanzania, Je! atumchagua nani?
Akijibu swali hilo, Diamond ametaja watu wawili na kueleza sababu kwanini anataka kukutana nao, watu hao ni..
1. Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Alisema, amewahi kukutana naye wakata hajawa Rais, hivyo angependa kukutana nae sasa hivi aone reaction ya Rais kwake kama itakuwa sawa na ile ya wakati wa kampeni au itakuwa ya namna gani.


2. Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Kampuni yaBakhresa Group, Said Salim Bakhresa. Alisema anatamani kujua ni namna gani mfanyabiashara huyu anaweza kufanikisha mambo yote anayoyafanya. Alisema Bakhresa ana biashara nyingi, lakini zote zinakwenda vizuri. Diamond alisema licha ya yeye kuwa mwanamuziki lakini pia anapenda kufanya biashara.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni