.

Jumanne, 2 Agosti 2016

DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU PICHA YA HAMISA MOBETO INAYOSAMBAA KWENYE MITANDAO


Baada ya mastori kibao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobeto anatoka na Diamond, Sasa Diamond amefunguka juu ya hayo.

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Diamond platnumz anayetamba na ngoma yake ya kidogo aliowashirikisha P square amejikuta akiingia kwenye duara zito la kuambiwa kuwa anatoka na mwanadada Hamisa Mobeto ambaye anasemakana kwa sasa yupo karibu na familia hiyo, Diamond ameamua kufunguka juu ya swala hilo kutokana na vitu vingi vinavyozungumzwa kuwa ni vya uwongo.


Kupitia kipindi cha leo tena kinachorushwa na Cloudsfm, kimepiga stori na Diamond platnumz juu ya swahilo, Diamond alifunguka kuhusu ishu hiyo na kusema kuwa chanzo ambacho kimefanya kutokea kwa yote hayo ni kutokana na ujio wa video yake mpya aliyomshirikisha Raymond ambayo mwanadada Hamisa Mobeto ametumika kama model.
“Ni watu ambao tunakuwa tunaheshimiana tu, sasa ndio hivyo na juzi kati hapa alikuwa kwenye video mpya hapa yangu niliyoshoot mimi na Rayvanny so yeye ni moja ya model aliyekuwepo kwenye hiyo video………..alafu hii pia ilichangia kuingiza maneno hapa kati, ndio mana watanzania wengi wanapenda kushoot video South Afrika kwasababu Bongo kunawambea wengi,…….uongozi wangu ndio waliomba awepo kwenye hiyo video..” Alisema Diamond platnumz.
Vilevile Diamond alizungumzia kuhusu picha ambayo imeonekana kwenye chumba ambacho Diamond alipiga picha, Zali na Hamisa wakiwa katika chumba kimoja.
“Pale ile sehemu inaitwa Capital, ni Appartment, appartment ambazo vyumba vyote vinafanana kama unavyoona vile….alafu watanzania wengi wanapenda kuingia pale ni pazuri halafu sio gharama kubwa…….ukiona picha yake ile ya Hamisa ni ya zamani kidogo kulingana na picha zetu tulizopiga mimi na zari, wakati mimi nikiwa south kila mtu anakuwa na kadi yake, kwahiyo sio rahisi Kufanya vitu hivyo..” Alismea Diamond Platnumz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni