Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways limesimamisha safari za ndege kuelekea nchini Sudan Kusini kufuatia machafuko mjini Juba.
Kupitia kwa mtandao wake wa kijamii wa Twitter , Kenya Airways inasema kuwa ''tunasikitika kusimamisha safari za ndege kuingia Juba kufuatia hali tete ya usalama jijini humo.
Tunaomba radhi kwa wale waliokuwa wanategemea kusafiri leo.
Hata hivyo tutawajuza hali ikibadilika''. taarifa ya Kenya Airways.
Hatua hiyo ya shirika hilo la ndege inafwatia taarifa kutoka Sudan Kusini zinazosema kuwa nasema mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni wanajeshi wameuawa katika mapambano baina ya vikosi vyenye uhasama katika mji mkuu wa Juba.
Mwandishi mmoja wa habari aliyeko mjini Juba amesema mapigano yameendelea mpaka mapema saa za asubuhi .
Wanajeshi wameonekana wakitembea mitaani huku watu wachache wakionekana kutoka nje.
Daktari mmoja amesema mili mingi imepelekwa hospitali huku chumba cha kuhifadhia maiti kikiwa kimejaa.
Awali Wanajeshi wanamuunga mkono makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar walisema kuwa kambi yao ilishambuliwa usiku wa kuamkia jana kwa risasi na bunduki nzito nzito.
Zaidi ya watu 100 wengi wao wanajeshi wanaripotiwa kuuawa mjini Juba wakati wa mapigano kati ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar
Wawili hao walikubaliana kumaliza vita vya wenywe kwa wenyewe na wametoa wito wa kuwepo utulivu.
Mapigano hayo yaliyoanza siku ya Alhamisi yaliendelea hadi mapema Jumamosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni