.

Jumapili, 17 Julai 2016

Sina tatizo na Hamisa Mobeto: Lulu


Kumekuwa na uvumi wa muda mrefu kwamba mastaa wawili wa tasnia ya filamu Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) na Hamisa Mobetto kwamba wana ugomvi mkubwa kwa chanzo kinacho semekana kuwa Lulu amemchukulia mwanaume msanii mwenzake huyo.

Ni miezi kadhaa imepita sasa toka ziripotiwe taarifa zisizo rasmi kuwa Lulu sasa hivi yupo katika mahusian ya kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wa mwanadada Hamisa Mobetto.

Hamisa Mobetto sasa ni mama wa mtoto mmoja, Mtoto ambaye amezaa na Mkurugenzi wa Efm Radio (Majizo) ambaye inasemekana kwa sasa yupo katika mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Lulu.

Lulu amehojiwa katika kipindi cha D’Wikend ChatShow kinachoruka Clouds TV kila siku za Ijumaa saa tatu usiku na kuulizwa kama ana tatizo na msanii mwenzake huyo na haya ndio yalikuwa majibu yake;

“Sina tatizo nae, labda sijui yeye kama ana tatizo na mimi ila mimi binafsi sina tatizo nae”Ndio jibu alilo wapa Soudy Brown na Qwhisar ambao ndio wana host kipindi hicho na kukanusha kabisa uvumi ulio enea mtaani kuwa yeye na Majizo wana uhusiano wa kimapenzi na akaomba watu waondokane kabisa na fikra hizo potofu na akadai kuwa uhusiano wa yeye na Majizo ni wa kikazi tu!

Elizabeth Michael Lulu alipata wasaa wa kuitambulisha rasmi movie yake mpya inayoitwa Ni Noma ambayo inatoka muda wowte kuanzia sasa! Kaa mkao wa kula

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni