.

Jumanne, 19 Julai 2016

Petit Man aijibu kauli ya Wema kuwa yeye ndiye sababu ya wasanii wa Endless Fame kutofanya vizuri


Aliyekuwa msimamizi wa wasanii walioko chini ya lebo ya Endless Fame ya mwanadada Wema Sepetu (PetitmanWakuache) ameijibu kauli liyotolewa na Wema Sepetu Jumatatu ya wiki iliyopita kuwa yeye (Petitman) ndio sababu ya wasanii wa lebo hiyo kushindwa kufanya vizuri.

Jumatatu ya Tarehe 11 mwezi huu Mwanadada Wema Sepetu alisikika kwenye 255 segment ya kipindi cha XXL kinachoruka Cloudsa Fm jumatatu hadi ijumaa saa 7 mchana hadi saa 10 jioni akitoa malalamiko yake kwa Petitman kuwa yeye ndio sababu ya wasanii wake kushindwa kufanya vizuri katika game ya muziki.

“Naweza kusema kwamba kwa sababu ni muda mrefu nilikuwa nimemuachia Petit hiyo kazi sidhani kama alikuwa anaitenda vizuri, kwahiyo let us give it another 3-6 months tusimame sisi kama sisi kwasababu unajua hivi vitu vya kum trust mtu anaweza kufanya tofauti na ulivyo tarajia”

Ni maneno aliyo yazungumza Wema Sepetu wiki iliyopita.

Perfect255 imemtafuta Petitman na kupiga nae story juu ya swala hilii na analipi la kuzungumza!

“Siwezi kuzungumzia kitu chochote zaidi ya kusema kwamba kauli zake nimezisikia na nimezipokea vizuri, makosa ni ya kwangu mimi, me naomba watanzania wanitizame kwa chansi niliyokuwa nayo kwa sasa hivi na wasanii wangu Billnass na Nuh watutazame spidi yetu itakapo fikia kisha wayanzania ndio watatoa jibu kama ni kweli nilikuwa nafelisha au nilikuwa nafelishwa.” Alisema Petitman Wakuache

“Kujituma ndio siri ya mchezo, msanii kabla ya meneja kuhangaika unatakiwa wewe mwenyewe kaka msanii ufuatilie kazi zako na vilevile uwe serious na muziki ambao wewe unaufanya! Lakini ukiwa na msanii ambaye hayuko serious na muziki anao ufanya hamuwezi kufika popote.”

Aliongeza Petitman Wakuache
Petitman sasa anafanya kazi na wasanii wawili wanaofanya vizuri kwasasa Billnass na Nuh Mziwanda.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni