.

Jumamosi, 9 Julai 2016

Nay wa Mitego ahofia ngoma ya “Pale kati Patamu” kufungiwa


Nay wa mitego aonyesha wasiwasi kuhusu wimbo wake mpya wa “Pale Kati Patamu” kufungiwa na Basata.

Msanii wa miondoko ya Hiphop Nay wa mitego ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Saka hela’ ameonyesha wasiwasi na kuhofia wimbo wake mpya ambao utatoka siku ya Jumatatu ya tarehe 11 kufungiwa.

Kupitia kurasa yake ya Instagram Nay The true Boy aliwataka mashabiki wake kushika tarehe ya siku ngoma yake itakapo toka kwani kilichoimbwa humo mpaka yeye anapagawa, na kuonyesha hofu kama ngoma hiyo italetewa zengwe.


“Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya.

‘Pale kati Patamu’ hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?” aliandika Nay.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni