.

Jumamosi, 9 Julai 2016

Mmiliki wa Twitter, Jack Dorsey amedukuliwa akaunti yake ya twitter


Mwezi na siku zake zilizopita tulishuhudia wasanii wa Bongofleva wakilalamika kudukuliwa akaunti zao na Hackers, Sasa CEO wa mtandao wa Twitter, Jack Dorsey’s amedukuliwa akaunti yake ya Twitter.

Jack Dorsey’s ni mmiliki wa mtandao wa twitter, hivi karibuni ameripotiwa kudukuliwa akaunti yake na kikundi cha Hacker’s ambao walidukua akaunti ya mmiliki wa Facebook (Mark Zuckerberg) pamoja na CEO wa kampuni ya Google Sundar Pichai’s.

Kikundi hicho cha wadukuzi kinachojulikana kama “Our Mine” kimekuwa ni tishio kubwa kwa wamiliki wa mitandao mikubwa huko nchini Marekani, Lengo lao kubwa huwa nikuonyesha udhaifu wa wamiliki hao kwenye maswala ya ulinzi kuhusu watumiaji wake ni kwamba wanaweza kufuta akaunti ya mtu yeyote yule.

Tukirudi nyumbani “Bongo” wadukuzi ambao wanadukuwa akaunti za wasanii wa Bongofleva haijulikani kama lengo lao haswa ni lipi, inaweza kuwa ni chuki au kuharibu status ya msanii? hakuna anayejua.

Kwa upande wa wenzetu hudukuliwa kutokana na kupima uwezo wako wa neno siri zako zina nguvu kiasi gani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni