.

Jumapili, 10 Julai 2016

Marufuku wanawake waislamu kufunika uso Rwanda


Wanawake waislamu nchini Rwanda,wapigwa marufuku wasijifunike nyuso zao.

Hatua hiii imechukuliwa na jumuiya ya waislamu nchini humo iliyofikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab linalovaliwa na wanawake.

Vazi hilo hufunika uso wote wa mwanamke.

Jumuiya hiyo imesema marufuku hiyo inatokana na sababu za kiusalama kwa waislamu na vilevile warwanda.

'' Hili vazi ni la kiislamu hata hivyo limeanza kutumika vibaya kwa madhumuni ya kudhuru usalama wa waisilamu na vitendo vinavyokinzana na mafunzi ya dini ya Kiislamu''

''Jambo la pili ni usalama wa nchi. kwa sababu watu wanajificha na kutenda vitendo pasi na kutaka kuonekana''.

''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa Sindayigaya.

Uamuzi huo umetokea wakati kundi la watu 17 wa kiislam wanazuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kutaka kujiunga na kundi la IS na kufundisha itikadi za kundi hilo.

Katika msikiti mkuu wa Nyamirambo jijini Kigali ni wakati wa swala ya adhuhuri,,,waislam wengi wanaingia msikitini …lakini huwezi kuona hata mmoja anayevaa niqab miongoni mwa wanawake au mabinti wanaoingia hapa msikitini

Wanawoiunga mkono kauli hiyo ya jumuiya ya waislam nchini Rwanda wanasema kuwa Niqab ilikuwa imeanza kutumika kuficha maoavu mengi katika jamii.

Aidha wanasema kuwa wanawake waislamu wanapaswa kuwajibika kwa kujiepusha na maovu ambayo sasa yameanza kuchipuka kwa kisingizio cha Niqab.

Kuna wengine walioghadhabishwa na uamuzi huo lakini hawakutaka kuzungumzia suala hilo wakisema wanahofia usalama wao.

Hapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi la Islamic State na pia kueneza itikadi za kundi hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni