.

Jumatano, 8 Juni 2016

Programu ya Apple Siri yaita ambyulensi kumsaidia mtoto


Mwanamke mmoja kutoka Cairns Australia,alitumia programu ya Apple Siri kupigia simu ambyulensi kwa mtoto wake wa mwaka mmoja alipokuwa na tatizo la kupumua.

Stacey Gleeseon alichukua simu yake aina ya iphone na kukimbia hadi chumba cha mtoto ili kumsaidia lakini akaiangusha simu hiyo alipowasha taa.

Alipiga kelele akiitaka simu hiyo kuamsha programu ya siri na kuiambia programu hiyo kuita huduma ya dharura huku akianza kumfufua mtoto huyo.

Bi Gleeson aliambia BBC kwamba anahisi huduma hio ingeokoa maisha ya mwanawe.

Aliamrisha siri kuita ambyulensi na aliweza kuzungumza na huduma hiyo ya dharura huku akimfufua mwanawe Giana.

Giana ambaye amekuwa akiugua maambukizi ya kifua alianza kupumua tena wakati ambyulensi hiyo ilipowasili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni