.

Alhamisi, 9 Juni 2016

TAS wazungumza haya kuhusu majina wanayoitwa watu wenye Ualbino

Image result for albino
June 09 2016 Chama cha watu wenye ualbino (TAS) wamekutana na vyombo vya habari ambapo wameeleza kuhusiana na siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino.
Siku hiyo ni June 13 kila mwaka na mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya 11 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka 2016 na ya pili kimataifa tangu baraza la umoja wa mataifa kuitangaza rasmi June 13 ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu Ualbino.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino (TAS) Nemes Tembo amezungumzia kuhusiana na majina ambayo wamekuwa wakiitwa watu wenye ualbino, majina hayo ni kama vile zeruzeru na watu wenye ulemavu wa ngozi……..
>>>’Zeruzeure ukiangalia hata kwenye kamusi wanahusisha na shetani au kitu kibaya na hata utakaposema mlemavu wa ngozi bado pia sio sahihi kwa sababu shida yake sio ngozi tu ila inatokana kukosekana kwa kemikali fulani  inayoitwa melanini katika ngozi na inayosbabisha rangi ya ngozi kuwa nyeupe, rangi kutokuwa nyeusi kama ilivyo kawaida na rangi ya nywele kuwa nyeupe au brown’
Aidha chama hicho kimesema kuwa silimia 90 ya watu wenye ualbino wanakumbana na tatizo la saratani ya ngozi na hata hivyo gharama za matibabu wengi wao wanashindwa kuzimudu hivyo wameiomba serikali kutenga bajeti ambayo itasaidia kupatikana kwa matibabu hayo kwa urahisi. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni