.

Ijumaa, 13 Mei 2016

Vitu 11 ambavyo hutakiwi kuvifanya ukiwa Dubai

Dubai ni moja ya miji ambayo kwa sasa watanzania wengi wanaenda kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali, sasa mtu wangu nimekutana na hivi vitu kumi na moja ambavyo hutakiwi kuvifanya ukiwa Dubai.

1. Kutojihusisha na shughuli za Madawa ya kulevya, inasemeka Dubai wako makini kwenye suala ya kupinga matumizi na uuzaji wa madawa ya kulevya huenda kuliko mji wowote.
2. Hutakiwi kunywa pombe kwenye maeneo ya Public.
3. Hutakiwi kuvaa bila Kujistiri, wanawake wanatakiwa kujiepusha na kutembea nusu uchi kwenye maeneo kama beach na hata wanaume wanatakiwa Kujistiri wakati wakitembea kwenye mitaa ya mji huo.
4. Hutakiwa kupiga muziki kwa sauti ya juu wala kucheza mpaka uwe katika maeneo ambayo ni maalum kwa shughuli hizo kama vile klabu.
5. Hauruhusiwi kukiss ukiwa public, wanandoa waingereza walifungwa kwa kufanya mapenzi beach lakini hata kiss inaweza kukuweka matatani.
6. Epuka maneno ya kufuru dhidi ya Uislamu.,wageni wengi wamekuwa matatani kwa sababu walikuwa wanajaribu kutoa maoni yao.
7. Kuwa mwangalifu na kamera yako, hauruhusiwi kupiga picha mtu picha bila idhini yake. 
 9. Kuwa mwangalifu na Wallet yako . Dubai imeelezwa kuwa na kiwango kidogo sana cha uhalifu lakini uhalifu mdogomdogo unajitokeza kama sehemu zingine.
10. Usile hadharani kipindi cha Ramadhani, hutakiwi kula, kunywa au kuvuta sigara wakati wa mfungo hata kutafuna Big G.
 11. Usitumie mkono wa kushoto kwa sababu mkono huo hutumika kwa ajili ya usafi wa mwili, usimsalimie yeyote kwa mkono wa kushoto, kufungua mlango wala usimpe mtu chakula kwa mkono wa kushoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni