.

Jumanne, 10 Mei 2016

Ommy Dimpoz aelezea kuhusiana na mahusiano yake

Wakati mwingine unaweza kufunguka juu ya hisia zako kwa mtu fulani ingawa wakati mwingine zinaweza kuathiri jamii; pamoja na kwamba mtu hakatazwi kueleza juu ya hisia zake hata kama jamii itatafsiri kwa upande hasi ama chanya. Unataka kujua Star wa Achia Body Ommy Dimpozy amesemaje?

DIMPOZY AELEZA HISIA ZAKE

Ommy Dimpoz amesema kuwa hapendi ku “date” na wanawake maarufu kwa kuwa  hakuna siri baina yenu hivyo anaepuka kuwa katika uhusiano na mtu maarufu, amesema kuwa kama asingekuwa maarufu angependa ‘ku-date’ na Star wa Bongo Movie Wema Sepetu.

“Ukidate na mtu maarufu there is no privacy  maana unaishi kwa filling za kuridhisha  marafiki  wa girl friend wako,  kama asingekuwa star ningetamani kudate na Wema” ameongeza Ommy Dimpozy

Ommy Dimpozy hivi karibuni amemtambulisha msanii kutoka katika Label ya PKP anayefahamika kwa jina la Nedy 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni