.

Jumanne, 31 Mei 2016

Man United wamefanya maamuzi mapya kuhusu hatma ya Marcus Rashford

Klabu ya Manchester United ya Uingereza jana May 30 2016 imetangaza maamuzi mapya ambayo yatawapa furaha mashabiki wa klabu hiyo, Man United jana May 30 imetangaza kumpa mkataba wa miaka minne kinda aliyekuja kwa kasi Marcus Rashford.

Man United wamempa mkataba huo wa miaka minne utakamuoweka staa huyo Old Trafford hadi June 2020, Rashford mara ya kwanza kucheza mechi na kikosi cha kwanza cha Man United alifunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya Midtjylland mwezi February.
UnitedÂ’s Marcus Rashford celebrates after scoring  during the Europa League round of 32 second leg soccer match between Manchester United and FC Midtjylland in Manchester, England, Thursday, Feb. 25, 2016 . (AP Photo/Jon Super)
Kutoka kushoto ni Marcus Rashford na Cameron Borthwick-Jackson waliposaini mikataba yao
Kinda huyo wa Man United amefanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 akiifungiaMan United jumla ya magoli 8 katika mechi 18 alizoichezea klabu hiyo msimu huu,Rashford kwa sasa ana umri wa miaka 18 na alianza kuichezea timu ya vijana ya Man United toka mwaka 2005, kinda huyo pia ameitwa katika kikosi cha England cha wachezaji 26 watakaoshiriki michuano ya Euro 2016.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni