.

Jumatano, 11 Mei 2016

Mafikizolo wameingia Dar es salaam usiku huu

Kundi maarufu la muziki kutokea Afrika Kusini Mafikizolo limewasili Dar es salaam Tanzania kwa ajili ya kujitangaza zaidi na kolabo yao waliyomshirikisha Diamond Platnumz colours of Africa‘ pamoja na kutumbuiza kwenye uzinduzi wa Internet ya 4G ya Vodacom Tanzania.

Kwenye majibu waliyoyatoa Airport,Mafikizolo wameishukuru Vodacom kwa kuwezesha Watanzania kuja kuona show yao bila kulipa kiingilio lakini pia wamesema kolabo yao na Diamond imekua ngoma kubwa kwao na wamefurahi kuona inapenya Afrika kwasababu hilo ndilo lilikua lengo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni