.

Jumamosi, 14 Mei 2016

KITAKACHOWAPA PESA NDEFU ALIKIBA NA DIAMOND PLATNUMZ

Kwa uchunguzi mdogo usio rasmi uliofanyika inaonekana kabisa ukiona kuna jambo linabishaniwa ujue kweli jambo lipo.

Kuhusu Ali Kiba na Diamond hakuna kuficha upinzani upo kweli na hawa ndio haswa wananogesha muziki wa Bongo Fleva. Kwa Tanzania kupambanisha watu watu imeanza zamani  mfano Msondo na Sikinde ama Nasma Hamisi na Hadija Kopa lakini hawakuwa na ugomvi, ilikuwa kwa ajili ya kupiga pesa na walipiga kweli pesa.

Kiba na Diamond Platnumz hawana bifu ila hawapendani kwa kuwa kila mmoja ana mafanikio yake na njia zake mbalimbali za“kutusua” wachukue uhasama huo ambao sio wa kweli wapige pesa kama ilivyofanyika katika tamasha lao moja lililofanyika Jijini Dar es Salaam.


Kitakachoweza kuwapa pesa nyingi ni kolabo tu wala sio kingine kwa kuwa kwa sasa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva wanakiu ya kuona jambo hilo likifanywa na wawili hao, isipokuwa ugumu wa hilo ni nani kumfuata mwenzake kukaa chini na kufanya mambo watu wanayotaka?, ila kama watafanya hivyo watapata matamasha mengi zaidi ambayo wataingiza pesa nyingi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni