.

Jumatatu, 9 Mei 2016

JUSTIN BIEBER ASHITAKIWA

Kumekuwa na matukio kadhaa ya uharibifu  ambayo yamekuwa yakifanywa na watu maarufu duniani, mwezi uliopita Mwanamuziki Justin Bieber alivunja simu ambayo ilisemekana mmiliki wake ni Robert Earl baada ya kujaribu kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa Pombe mjini Texas.

Kulingana na taarifa za mtandao wa TMZ, Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu hiyo na kuivunja, baada ya tukio hilo msanii huyo alishtakiwa na kutakiwa kulipa kiasi  cha Dola za Kimarekani milioni 100,000 ambapo Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu taarifa hizo hadi sasa.
Sababu iliyopelekea Bieber kuchajiwa kiasi kikubwa cha fedha ni kutokana na simu hiyo kuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni