.

Jumanne, 24 Mei 2016

Hii ndiyo sababu ya Big Brother kutofanyika mwaka huu


Mashabiki wa mashindano ya Big Brother Africa wameachwa njia panda baada ya tarifa kutolewa rasmi kuwa mashindano hayo hayatakuwepo mwaka huu.
Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Afrika, huku Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano hayo hapo mwakani.
“We wish to thank Big Brother Africa fans far and wide for their continues support over the past edition and promise that the show will go on on Dstv, with new and excting productions in store from M-Net,” wamesema.
Mpaka sasa taji hilo la Big Brother linashikiliwa na Idris Sultani aliyefanikiwa kushinda mwaka jana na kupata zawadi ya fedha kiasi cha dola laki tatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni